WILAYA ya Kibaha iko mbioni kujengewa Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) baada ya mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini, Silvestry Koka kutoa msaada wa mifuko 100 ya saruji kufanikisha ujenzi huo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Julai 7, 2023 wilayani hapa, mbunge huyo alisema uamuzi huo umetokana na baraza hilo kukosa ofisi katika wilaya tajwa.
Alisema ujenzi wa ofisi hizo zitasaidia Bakwata kuendesha shughuli za kutoa huduma Kwa jamii bila changamoto yoyote .
“Bakwata walinieleza wanakabiliwa na changamoto ya ofisi niliwaahidi mifuko 100 ya saruji na Leo hii nimekuja kutimiza ahadi yangu kwani jukumu langu ni kuisaidia jamii ikiwemo taasisi mbalimbali hususani hizi za dini.”Alisema Koku.
Aidha ameitaka jamii na taasisi binafsi kujijengea utamaduni wa kutoa msaada kama sadaka kwa maeneo yenye uhitaji hatua ambayo itaisaidia kuharakisha maendeleo na kutatua kero zilizopo.
“Mimi nitasimama nanyi kuhakikisha ujenzi huu unakamilika vizuri hivyo nitoe wito kwa watu wengine kujiwekea utaratibu wa kutoa Sadaka kusaidia changamoto kama hizi na zile zinazoikabili jamii Sadaka ukiitoa Kwa moyo mwenyezi Mungu atakuzidishia.”aliongeza
Shehe Mkuu Wilaya ya Kibaha Saidi Mtonda, amesema ujenzi wa ofisi hiyo unatarajiwa kugharimu zaidi ya milioni 70 na kwamba bado fedha zaidi zinahitajika ili kifanikisha ujenzi huo.
“Tunaishukuru tumepata saruji hii kutoka kwa mbunge itaisaidia kunza ujenzi wa ofisi yetu hivyo tunaomba watu wengine wenye Nia njema waendelee kujitokeza na kutusaidia maana jumla milioni 70 zinahitajika.”alisema
Comments are closed.