WACHEZAJI wa Simba SC, Mzamiru Yassin na Kibu Dennis wamepigwa faini ya Sh milioni 1 kila mmoja kwa kosa la kuondoa taulo la mlinda mlango wa Coastal Union, Ley Matampi.
Taarifa iliyotolewa leo na Bodi ya Ligi (TPLB), imeeleza kuwa kitendo hicho kiliashiria imani za kishirikina.
Katika mchezo huo uliopigwa Machi 9, Simba SC ilipata ushindi wa mabao 2-1 uwanja wa Mkwakwani Tanga.