Kiduku, Mandonga kilio
UMEKUWA usiku wa machungu kwa wapenzi wa ndondi nchini baada ya bondia Twaha ‘Kiduku’ kupigwa na mpinzani wake kutoka Afrika Kusini, Asemahle Wellem katika pambano la raundi 12 kuwania mkanda wa ubingwa wa mabara unaotambuliwa na Shirikisho la Masumbwi la WBF.
–
Wellem alipata ushindi wa pointi kwa majaji wote watatu, ambapo Kiduku amesema baada ya mchezo kuwa mpinzani wake alikuwa bora kuliko yeye na kuwaomba radhi mashabiki wake akiahidi kuangalia wapi alikosea na kufanya vizuri siku zijazo.
–
Naye bondia Karim Mandonga amepoteza pambano lake kwa TKO katika raundi ya tatu dhidi ya mpinzani wake Moses Golola, pambano lililofanyika usiku wa kumkia leo jijini Mwanza.