Kiduku, Sebyala ulingoni Disemba 26

Bondia Twaha Kassim ‘Kiduku ‘ anatarajia kupanda ulingoni dhidi ya bondia kutoka Uganda Mohamed Sebyala katika pambano la usiku wa mabibgwa litakalofanyika Desemba 26, mwaka Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Kiduku alisema
kuwa anarudi kivingine baada ya kupoteza pambano lake liliilopita dhidi ya bondia kutoka Afrika Kusini.

“Baada ya kupoteza pambano lililopita sasa ninarudi kwa kasi nyingine na kwa hamu ,hivyo niseme tu mpinzani wangu amekanyaga nyoka mkia tukutane Disemba 26 mwaka huu,” alisema Kiduku.

Advertisement

Kwa upande wake, Mratibu wa matukio wa Kampuni ya Peak Time Media ambao ndio waandaaji, Bakari Khatibu, alisema kuwa lengo ni kusherehekea na kutambua mchango kwa mabondia walifanya kazi nao kwa muda mrefu.

“Kuelekea pambano hilo lililobeba kauli mbinu wanyama wamerudi nyumbani mabondia watakaopanda siku hiyo wamesaini mikataba yao na tunatarajia kufanya zoezi la kupima afya Disemba 12,” alisema Khatibu.

Aliwataja mabondia wengine watakaopanda ulingoni siku hiyo kuwa ni Oscar Richard dhidi ya Sabelo Ngebinyana ( Afrika Kusini), Saidi Bwanga dhidi ya Fransis Miyeyusho,
Maono Ally dhidi ya Joseph Maigwisa na Sara Alex dhidi ya Jesca Mfinanga.

Wengine ni Hasan Ndonga dhidi ya Gabriel Ochieng (Kenya), Ally Ngwando dhidi ya John Chuwa, Charles Tondo dhidi ya Nick Otieno (Kenya), Tampera Maulus dhidi ya Waziri Magombana,
Saidi Tores dhidi ya Richard Mkude na Vigulo Shafii atapewa mpinzani baadaye.

Naye Mjumbe wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) Abdallah Juma,alisema kuwa wamebariki pambano hilo huku akiipongeza Peak Time kwa kufanya kazi nzuri za kuibua vipaji vingi vya ngumi.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *