Kiduku: wamemkanyaga nyoka mkia

DAR ES SALAAM: HAYAWI hayawi, punde kuwa na usiku wa deni haukawii kuwika.

Bondia kipenzi cha wapenda ndondi nchini, Twaha Kassim ‘Kiduku’ leo katika usiku wa ubingwa ‘boxing on boxing day’ atakiwasha ulingoni dhidi ya bondia kutoka Uganda Muhammad Sebyala ‘Medi Kabona’ katika Ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam.

Mratibu wa pambano hilo, Meja Selemani Semunyu amewataka mashabiki wa ndondi kufanya hima ili kuwahi tiketi kwani muitikio ni mkubwa.

“Ubungo Plaza itafurika tiketi za elfu kumi ‘sold out’ zimekwisha kazi kwako sasa ni elfu thelathini VIP Na elfu hamsini VVIP,” amesema Semunyu.

Akiongea kuelekea katika pambano hilo la round 10 lisilo na ubingwa, Kiduku amesema anaenda kurejesha heshima.

 

“Wamemkanyaga nyoka mkia, naenda kusafisha palipochafuka.” Amesema bondia huyo wa Morogoro.

Naye, Medi Kabona amesema amekuja Tanzania kwaajili ya shughuli moja tu “kumpiga bwana Twaha.” Ametamba Kabona.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button