Kidunda amtangazia maumivu mpinzani wake

BONDIA Seleman Kidunda, ametamba kumpiga KO ya raundi ya tatu mpinzani wake Patrick Mukala raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Mabondia hao watapanda ulingoni Ijumaa wiki hii kuwania mkanda wa ABU Ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam.

Akizungumza na HabariLEO, bondia huyo, amesema kinachompa jeuri ni maandalizi mazuri ambayo ameyapata chini ya kocha wake Habibu Kinyogoli ‘Master’.

Advertisement

“Nimemfatilia mpinzani wangu ni bondia mzuri, lakini mbinu alizonipa kocha wangu na mazoezi ambayo naendelea kuyafanya vinanipa uhakika wa kushinda pambano katika raundi ya tatu na kuondoka na mkanda huo wa ABU,” amesema.

Pambano hilo litakuwa la raundi 10 uzito wa Super Middle na litatanguliwa na mapambano tisa ya utangulizi.