Kifo cha mjamzito Kabuku chanzo wahudumu wa afya

TANGA: Tume iliyoundwa na Waziri wa afya, Ummy Mwalimu kuchunguza kifo Cha mjamzito, Marium Zahoro imebaini kuwa kifo hicho kilitokana na uzembe wa wataalamu wa afya na sio kutokana na kukosa fedha za matibabu kiasi cha Sh. 150,000.
 
Kifo cha Marium Zahoro kilitokea mnamo Novemba 11 katika kituo cha afya cha Kabuku baada ya kushindwa kujifungua kwa njia ya kawaida na kuhitaji kufanyiwa upasuaji na kuchelewa kwa huduma ya dharura ya upasuaji.
 
Akiongea katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika kituo cha afya cha Kabuku, Waziri Ummy amesema kuwa tayari baraza la madktari pamoja na waguuzi na wakunga linaendelea na utaratibu wa kuchukuwa hatua za kinidhamu kwa wataalamu wawili wa afya katika kituo hicho.
 
“Tutahakikisha baada ya hili hakuna kifo kinachotokana na uzembe kinatokea hapa nchini kwani tumejipanga kuchukuwa hatua kali Ili iwe fundisho kwa watumishi wa afya wazembe”amesema Waziri Ummy.
 
Aidha akiwasilisha taarifa ya tume hiyo , Mwenyekiti wa tume Dkt Ali Said amesema kuwa chanzo cha kifo cha Marium ni kutokana na uzembe wa wataalamu hao kushindwa kuchukuwa hatua za haraka ili hali mgonjwa akiwa katika hali ya hatari.
“Marehemu Marium alichelewa kupatiwa huduma ya upasuaji kutokana na kukosekana kwa mtaalamu wa dawa ya usingizi ambaye hakuwa anapatikana huku Daktari wa upasuaji kushindwa kutoa maamuzi ya Rufaa kwa wakati kwenda kwenye hospitali ya wilaya”amesema Dkt Said.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button