Kigogo walia mafuriko

DAR ES SALAAM, Wakazi wa Kigogo Kati jijini Dar es Salaam wamelalamikia kero ya mto kibanga kuleta maafa kwa wakazi wa eneo hilo.

Maafa hayo huletwa na mvua zinazoendelea kunyesha ambapo uacha njia yake ya asili na kukujaa kwenye makazi ya watu.

Miraji Simba mkazi wa eneo hilo ameelezea jinsi mto huo unavyoathiri maisha yao na kushauri serikali kuchukua hatua ili kuzuia maafa hayo yanayowakumba.

” Mto huu bila kingo bado athari itakuwa endelevu leo watakuwa wamepona hawa kesho wengine wako kwenye matatizo,” amesema Simba

Kwa upande wa Mwenyekiti wa serikali za Mtaa Kigogo Kati, Rashid Ally amesema hatua za awali walizochukua kupunguza athari za mvua kwa wananchi wa eneo hilo ni kuondoa takataka katika mto pamoja na kutaadharisha wananchi kutafuta hifadhi kwa muda ili kunusuru maisha yao.

Habari Zifananazo

Back to top button