MWENYEKITI wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Mufindi Kusini, David Kihenzile amechangia sh milioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Kata ya Igowele Mufindi Kusini.
Kiasi hicho kimejumuisha fedha taslimu ambazo ni sh milioni 5 na bati 120 zenye thamani y ash milioni 5 ikiwa ni kuunga mkono ujenzi huo ambao hadi kumalizika kwake utagharimu sh milioni 29.
Kihenzile, ametoa mchago huo katika kikao cha pamoja cha viongozi wote wa Kata hiyo wakiwemo wajumbe wa Mkutano Mkuu CCM Kata, Mabalozi, , Viongozi wa dini, Wafugaji, Wavuvi, Wazee w Mila, Watumishi wa Serikali pamoja na makundi mengine muhimu.
Aidha, katika kikao hicho pamoja na mambo mengine alifafanua kazi zilizofanyika na zinazoendelea kufanyika kwenye Kata hiyo ikiwa ni pamoja na mradi wa maji, ujenzi wa shule mpya sita, upanuzi na utoaji vifaa vya hospitali ya wilaya pamoja na ujenzi wa barabara ya lami za Nyololo na ile ya Mgololo.
Kihenzile anaendelea na ziara jimboni mwake ikiwa ni kusikiliza kero za wananchi na kuanzisha programu ya kujenga Chama kwa kuendelea kuhamasisha ujenzi wa ofisi na kuanzisha mkakati wa ugawaji Kadi za CCM 50,000 kwa mabalozi wa Shina.
Comments are closed.