Kihenzile: Wanaokwamisha Miradi kukiona

DAR ES SALAAM: NAIBU Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile amesema serikali haitofumbia macho Sekta yoyote itayokuwa kikwazo kwa wawekezaji katika maeneo mbalimbali.
Kihenzile ameyasema hayo leo Septemba 26, 2023 wakati wa ziara yake ya kikazi katika Bandari ya Dar es Salaam na kujionea namna shughuli mbalimbali zinavyofanyika pamoja na kukagua miradi inayoendelea kutekelezwa.
Amesema nia ya Serikali ni kuhakikisha uwepo wa Mazingira rafiki kwa Wawekezaji ili kufikia adhima ya Taifa kunufaika katika Uwekezaji huo.
“Maelekezo ya Rais Samia ni kuondoa kero, sasa ukiongeza kero ni kama unapingana na Rais, tunataka kila sekta kupunguza au kuondoa kabisa kero ili kuvutia zaidi wawekezaji” amesema Kihenzile.
Ameongeza Rais Samia anataka kuboresha Sekta ya Bandari na ndio maana maeneo mbalimbali katika Bandari ya Dar es salaam yameshaanza kufanyiwa maboresho, lengo likiwa ni kuvutia watu wengi zaidi kutumia Bandari za hapa nchini.

“Moja ya sehemu ya maboresho hayo ni kwamba tutasimika mitambo mkubwa zaidi ya kisasa kupima kiasi cha mafuta yanazoingizwa hapa nchini, Tunataka kuona Bandari zetu zikileta mapato makubwa, tukapeleke umeme vijijini, tukajenge Zahanati na huduma nyingine za kijamii”.

amesema

Aidha Kihenzile ameitaka Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kukamilisha kwa wakati miradi inayoendelea kutekelezwa kwa maslahi ya taifa.
“Nimeona kasi ya miradi mingi, mfano mradi wa Bagamoyo ni mkubwa sana, nmeona pia Mradi wa Mtwara, ombi langu kubwa kwenu wekeni kasi ya kutosha kwenye utekelezaji wa Miradi hii ili ikamilike, lakini pia umakini katika thamani ya Miradi hiyo.

“amesema kihenzile.

Habari Zifananazo

3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button