KIJANA Ansele Sebuka (42), mkazi wa Namagondo wilayani ukerewe, mkoani Mwanza amekutwa ndani ya chumba chake akiwa amejikata sehemu zake za siri kwa kutumia kisu kikali.
Polisi mkoani Mwanza katika taarifa yake imeema Sebuka alikuwa na ugomvi na familia yake, hali iliyomsababishia msongo wa mawazo, hivyo kusababisha kutaka kujiua kwa kujikata na kisu.
Inadaiwa Sebuka alikuwa anatuhumiwa na nugu zake kwa wizi wa mali mbalimbali za familia, pamoja na jamii inayomzunguka na kwenda kuziua, huku pia akituhumiwa kwa ulevi uliokithiri, hivyo familia kuamua kumtenga.
Taarifa ya polisi imesema kutokana na tuhuma hizo ndipo alipoamua kukata sehemu zake za siri kwa kisu chenye makali na kuacha zikining’inia, lengo ikiwa ni kujiua.
Sebuka alikimbizwa Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe kwa ajili ya matibabu na Polisi imesema anaendelea vizuri.