Kikao SEAJAA kufanyika Arusha
KIKAO cha Watendaji Wakuu wa Mahakama wa Nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika (SEAJAA) kitafanyika Oktoba 22, 2023 Jijini Arusha
Akiongea na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Chama cha Watendaji Wakuu wa Mahakama wa Nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika (SEAJAA) Profesa Elisante ole Gabriel ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, amesema maandalizi ya kikao cha watendaji hao yanaendelea kabla ya Mkutano utakaofunguliwa Oktoba 23 na Rais Samia Hassan Suluhu.
Alisema ushirikiano huo kati ya maofisa hao ndio unaosababisha ufanisi zaidi katika utoaji wa haki na utendaji kimahakama
Profesa Gabriel amesema kikao cha 13 zimejiunga na chama hicho huku jitihada za nchi nyingine tatu kujiunga na chama hicho zikiendelea na badae idadi ya wanachama wengine itaongezeka kufika Afrika nzima
“Ushirikishwaji wa masuala mbalimbali ni mojawapo kati mambo muhimu na kikao hiki kinatangulia kikao cha majajai wakuu na kitasaidia mijadala yake kushauri majaji wakuu katika masuala ya miundombinu,rasilimali watu na masuala ya fedha”
Amesema kikao kazi hicho kitajadili mambo mbalimbali kwani watendaji wakuu wanawashauri majaji wakuu katika masuala ya miundombinu, rasilimali za watu na masuala ya fedha
Pia kitakuwa na ajenda za marekebisho ya katiba ya chama hicho ikiwemo uboreshaji wa vyanzo vya fedha, uboreshaji wa mtandao wa chama hicho, mikakati ya masuala ya fedha huku nchi 13 za umoja huo zitakazoshiriki mkutano huo ambazo ni Angola, Botswana, Lesotho, Zanzibar, Shelisheli, Zimbabwe, Malawi, Msumbiji, Eswatini, Zambia, Namibia na mwenyeji Tanzania.