Kikeke kusherehesha tamasha la Simba

KUELEKEA Kilele cha Siku ya Simba Agosti 6,2023 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa Klabu hiyo imethibitisha kuwa Mshereheshaji namba moja wa tukio hilo ni Salim Kikeke.

Kupitia mitandao yake ya kijamii leo Agosti 5, Simba imethibitisha kuwa  Mtangazaji huyo wa zamani wa shirika la Utangazi la nchini Uingereza (BBC) ndiye mwenye jukumu la kusherehesha katika tamasha hilo.

“Kutoka London Hadi Dar Es Salaam, Salim Kikeke atakuwa MC namba moja kwenye tamasha kubwa Nchini” imeeleza taarifa hiyo

Katika kuipamba siku hiyo Simba itacheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Power Dynamos ya Zambia.

Habari Zifananazo

Back to top button