Kikongwe auawa kwa imani za kishirikina Geita

KIKONGWE mwenye umri wa miaka 70 mkazi wa kijiji cha Mwenegezi wilayani Geita, ameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani na watu wasiojulikana wakimtuhumu ni mshirikina.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Berthaneema Mlay amethibitisha taarifa hiyo na kueleza hadi sasa watu sita wanashikiliwa kwa uchunguzi wa tukio.

Amesema tukio lilitokea Aprili 24, 2023 majira ya saa tatu usiku, huko katika Kijiji cha Mwenegezi, Kata ya Nyakagomba na mwili wake umefanyiwa uchunguzi na umekabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi.

“Watu walikuwa na imani za kishirikina wakimtuhumu kwamba ni mchawi, kwa hiyo kwa hatua za haraka zilichukuliwa na watu sita wakiwemo wanawake wawili na wanaume wanne wanashikiliwa,” amesema

Kamanda Berthaneema amewataka wananchi kuachana na imani potofu na kumrejea Mungu kwa kuwa imani potofu imekuwa kiini cha matuko mengi mkoani Geita, hali inayohatarisha amani na usalama.

Habari Zifananazo

Back to top button