Kikwete afika msibani kwa Msabaha

DAR ES SALAAM: Rais Mstaafu Dk Jakaya Kikwete ameungana na ndugu, jamaa na marafiki kwenye mazishi ya aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Ibrahim Msabaha (72) aliyefariki dunia Jumanne, Februari 13, 2024.

Mazishi hayo yamefanyika nyumbani kwa marehemu huko Kibaha, mkoa wa Pwani.

Marehemu Dk Msabaha alifariki dunia akiwa njiani akipelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya hali yake kubadilika ghafla ikiwa ni siku chache tangu atoke Hospitali hapo alikokuwa amelazwa.

Aidha, Dk Msabaha amewahi kuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mbunge wa Kibaha, mkoani Pwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Habari Zifananazo

Back to top button