Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dk. Jakaya Kikwete, amesema vyuo na taasisi nyingine za elimu nchini ni nyenzo muhimu kwa ustawi na maendeleo ya nchi kwa kuwa kazi ya taasisi hizo ni kuendeleza rasilimali watu na bila hivyo nchi haiwezi kuendelea.
Kauli hiyo ameitoa leo Julai 6, 2023 alipofanya ziara katika mabanda ya mashirika na taasisi za kiserikali na binafsi, ikiwa lengo ni kujionea kazi na bidhaa mbalimbali zilizopo katika Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara ‘Sabasaba’ yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
“Vyuo kazi yake ya kwanza kufundisha na vinafundisha, moja ya kazi kubwa ili nchi iweze kuendelea ni rasilimali watu na rasilimali watu inazalishwa katika elimu,” amesema.
Amesema shule kuanzia za msingi, sekondari, vyuo vikuu, vyuo vya mafunzo ya amali, vikifanya vizuri tunapata rasilimali watu wenye viwango ambao hutumika viwandani, hospitalini, mashambani na maeneo mengine ya uzalishaji na huduma.
Comments are closed.