Kikwete roho kwatu kwenye muziki

RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete amesema yeye ni mpenzi wa muziki na kwamba anapenda kuimba.

Akizungumza katika kipindi cha Leo Tena cha Clouds  mapema leo Oktoba 7, 2022 wakati wa kusherehekea miaka 72 ya kuzaliwa kwake, Kikwete alisema amekuwa mpenzi wa muziki tangu enzi za utoto wake.

“Napenda muziki, yaani sikio langu hili muziki wa aina yoyote ule huwa nauenjoy (nafurahi). Nikienda China mziki wa kichina nauenjoy, wa kijapani, wakikorea, wowote ule. Kwahiyo mi kwenye muziki niko all round (kote),” alisema Kikwete.

Akifafanua kuhusu mapenzi yake kwa mziki, alisema kuwa moja ya mizigo ambayo akisafiri huwa ni lazima aibebe ni CD za nyimbo za waimbaji mbalimbali.

“Mi mapenda kuimba na nyimbo nyingi nazijua, za kina Cris Brown…when it comes to music nina passion hiyo, na ni mziki wote, taarab…,” alisema Kikwete na kuongeza:

“Mimi burudani yangu kubwa ni mziki, ninapopumzika nasikiliza mziki, napokuwa stressed nakwenda kwenye mziki tuu.”

 

Habari Zifananazo

Back to top button