Kikwete: Usalama wa nchi unaletwa na uhusiano mzuri

Kikwete: Usalama wa nchi unaletwa na uhusiano mzuri

RAIS mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete amesema uhakika wa usalama wa nchi unatokana na uhusiano mzuri na nchi nyingine duniani.

Kikwete ametoa kauli hiyo mapema Aleo, wakati wa maadhimisho ya miaka 10 ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC), kilichopo Kunduchi, Dar es Salaam, huku akisisitiza njia bora ya kuwa salama ni kuhakikisha kuwa hakuna uadui. .

“Lazima ufanye kila linalowezekana, ili kufanya nchi zote duniani kuwa marafiki zako. Hapo ndipo unaweza kuwa na uhakika wa usalama na ulinzi wako.

Advertisement

“Wakati mwingine hata hutakiwi kuhangaika kununua vifaru vya jeshi kwa sababu huna wa kupigana naye. Hakuna tishio kutoka nje,” Rais huyo mstaafu alisema.

Zaidi ya hayo, alisisitiza juu ya umuhimu wa sera nzuri isiyobagua na kuwanyima watu uhuru wao kama njia nyingine kuu ya kulinda usalama wa nchi.

 “Usalama wa nchi unahusisha mambo mengi, JWTZ ina jukumu la kulinda mipaka yetu, tuna huduma ya upelelezi ambayo ina jukumu la kupekua mambo yanayotokea duniani kote na kipengele kingine kikubwa kinachohusika ni sera nzuri ya ndani.

“Sera zinazolenga na kuwanyima watu uhuru wao hutengeneza mazingira ya nchi kutokuwa salama,” aliongeza Kikwete.

Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) kilianzishwa kikiwa na lengo kutoa mafunzo kwa maofisa.

 

1 comments

Comments are closed.