Kila baada ya dakika 8 mwanamke mmoja hufariki kwa kutoa mimba

KILA baada ya dakika nane, mwanamke mmoja hufariki dunia kutokana na utoaji mimba.

Hii ni licha ya viwango vya vifo vinavyosababishwa na matatizo ya uzazi kupungua kwa theluthi moja katika miaka 20 iliyopita.

Akizungumza katika Kongamano la wadau wa masuala ya Afya ya Uzazi lililoandaliwa na Chama cha Wanasheria Wanawake Tawla, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili(MUHAS), na bingwa wa magonjwa ya wanawake, Profesa Andrea Pembe amesema wanawake katika bara la Afrika ndio wanaongoza kufariki kwa hutoaji mimba usio salama.

Amesema, katika kila dakika moja kuna wamama wanne wanatoa mimba kwa njia ambazo sio salama.

“Na katika kila dakika 8 basi kuna mama ambaye anafariki kutokana na utoaji mimba. Wengine wanashindwa kupata ujauzito kwa sababu ya matatizo ambayo yametokana na utoaji mimba.”Anasema

Anasema wanawake milioni 56 utoa mimba duniani. Watatu kati ya wanne wapo bara la Afrika ambapo wanawake hao wapo hatarini zaidi kupoteza maisha  ukilinganisha na mabara mengine.

“Lakini si suala la kufa peke yake katika kila mama mmoja anakufa wengine upata matatizo ya muda mrefu kama ugumba.

“Duniani kwa ujumla unaweza kusema mwaka 2014 kulikwa na jumla ya utoaji mimba usio salama kwa wanawake million 42 na kati ya hizi nyingi zipo bara la Afrika.”

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) viwango hivyo  vilipungua pakubwa kati ya mwaka 2000 na 2015. Lakini vilisimama kwa kiasi kikubwa kati ya mwaka 2016 na 2020. Katika mataifa mengine hali ilidorora na kurudi nyuma.

Kwa jumla viwango vya vifo vya kina mama vilipungua kwa asilimia 34.3 katika kipindi cha miaka 20 kutoka vifo 339 kati ya wajawazito 100,000 mnamo mwaka 2,000 hadi vifo 223 katika mwaka 2020.

Licha ya sheria kukataza utoaji mimba, vitendo hivyo hufanyika na mara nyingi kwa njia zisizo salama

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button