Kila siku watu 200 huambukizwa VVU Nchini

DAR ES SALAAM: Kwa mujibu wa takwimu ya Ripoti ya viashiria vya maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI ya mwaka 2016/2017 inaonesha kuwa kila siku nchini Tanzania, watu 200 huambukizwa VVU.
Kati yao asilimia 40 ni vijana wenye umri kati ya miaka 15-24, hata hivyo vijana wakike wanaongoza katika maambukizi hayo kwa asilimia 70-80.
Hayo yameelezwa na Mwezeshaji kutoka Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dk. Patrick Kanyamwenge kwa niaba ya Mratibu wa TACAIDS Mkoa wa Dar es Salaam, Hafidh Ameir katika semina wezeshi kuhusu elimu ya UKIMWI kwa watumishi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tawi la DUCE, Temeke-Dar es Salaam.
Aidha, mwezeshaji huyo amesema malengo ya sasa ya nchi ni kuhakikisha ifikapo 2025 inafikia malengo ya dunia ya 95, 95, 95 (asilimia 95 ya watanzania wawe wamepima na kutambua hali zao, asilimia 95 ya waliogindulika na VVU wawe wameanza kutumia Dawa za kufubaza makali ya VVU, na asilimia 95 ya wanaotumia dawa wawe wamefubaza makali ya VVU)
Hata hivyo, Dk. Kanyamwenge amewaasa watumishi hao kuhakikisha wanajilinda na kuwalinda wengine na maambukizi dhidi ya VVU, pia kutoa elimu kwa watanzania.

Habari Zifananazo

4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button