Kilimo cha muhogo kuzalisha ajira 100,000

LINDI: SERIKALI imetoa ekari 62,000 za ardhi kwenye vijiji vinne katika Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi kwa Kampuni ya Pan Tanzania Agriculture Development kwa ajili ya uwekezaji wa kilimo cha mihogo ambao unatarajiwa kuzalisha ajira 100,000 kwa Watanzania.
Pia, uwekezaji huo wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 640 ambao ni sawa Sh trilioni 1.6 utahusisha ujenzi wa kiwanda kwa ajili ya uchakataji wa mazao yatakayozalishwa ili kuongeza tija, thamani na utanufaisha wakulima 10,000 kwa kupata mafunzo juu ya mazao hayo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo alieleza hayo jana katika makabidhiano ya eneo la mradi wa mwekezaji huyo linalohusisha Kijiji cha Mavuji, Migeregere, Liwiti na Nainokwe mkoani Kilwa chini ya Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA).
Awali, Profesa Kitila alisema serikali inatoa ardhi ekari 62,000 ambayo ni maliasili ya Watanzania lakini katika kutoa ardhi hiyo, wananchi hususan wakazi wa Kilwa watanufaika kwa kupata ajira kama ilivyoelezwa na kuongeza tija na ndiyo maana Tiseza inasimamia ili Watanzania wanufaike na uwekezaji.
“Tutawakabidhi maeneo wawekezaji na mfanye uwekezaji na msipofanya hivyo, tutawanyang’anya maeneo hayo bila woga na kukabidhi kwa wawekezaji wengine.
Tunataka kuhakikisha uwekezaji unazalisha ajira na kama tulivyosikia huyu atazalisha ajira 100,000,” alisema. “Si tu mihogo lakini uwekezaji huu unatarajiwa kuboresha kilimo cha maharage ya soya, korosho na uchakataji wa nyama. Vyote hivyo vitachakatwa na kwenda kuuzwa nje ya nchi,” alieleza.
Alisema mradi huo utasaidia kuongeza mapato kwa serikali kutokana na kodi, pia Sh trilioni 1.6 zilizowekezwa zitaongeza pato na thamani kwa Mkoa wa Lindi. Mkurugenzi Mtendaji wa Tiseza, Gilead Teri alisema mwekezaji asipotekeleza mradi wake, ardhi hiyo ipo chini ya mamlaka na itarejeshwa na kupewa kwa mwekezaji mwingine.
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo ya uwekezaji, Dior Feng alisema alama hiyo inaashiria kutimia kwa ndoto ya miaka saba iliyobeba matumaini ya kutatua changamoto ya kilimo kwa kuanzishwa kwa kilimo cha kisasa cha mihogo na mfumo wa kusafirisha bidhaa nje ya nchi, ahadi ambayo imetimia.
“Tunaanza mara moja uwekezaji wetu wa miaka 10 wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 640 kwa ajili ya kujenga upya miundombinu ya kisasa ya kilimo, kituo cha teknolojia na mfumo wa kusafirisha bidhaa nje ya nchi utakaovutia zaidi ya viwanda 80 kutoka China,” alisema Feng.
Katika hatua nyingine, Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Abdallah Nyundo alisema watu wa Kilwa na Mkoa wa Lindi kwa ujumla wamejiandaa kimkakati na wamejipanga kwa ajili ya uwekezaji, kwani ni mambo mengi yamefanyika kuchochea uwekezaji katika mkoa huo.
Baadhi ya mambo hayo ni uboreshaji wa nishati ili kuhakikisha kunakuwa na umeme wa uhakika ili kuvutia wawekezaji, ujenzi wa Bandari ya Kilwa unaotarajiwa kuzinduliwa mwanzoni mwa mwaka na uboreshaji wa barabara kuhakikisha zinafanya kazi nyakati zote.




I make up to $90 an hour working from my home. My story is that I quit working at Walmart to work online and with a little effort I easily bring in around $40h to $86h… Someone was good to me by sharing this link with me, so now i am hoping i could help someone else out there by sharing this link…
.
More Details For Us→→→→→→→→→ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com