Kilio cha Wananchi Kilosa chasikika Serikalini

MOROGORO: WANANCHI zaidi ya 10,000 wanaioshi Kata  ya Kisanga, Ulaya na Mikumi wilayani  Kilosa , Mkoa wa   Morogoro wataondokana na kero iliyodumu zaidi ya miaka minne ya kukosekana kwa daraja la kudumu katika mto Mfilisi  kijiji cha Iyombwe baada ya serikali kutoa Sh milioni 500 na kuanza ujenzi wa daraja hilo kwa ajili ya kuharakisha huduma za  maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Meneja wa Wakala wa Barabara za mjini na vijijini (TARURA) Wilaya ya Kilosa ,Mhandisi Harold Sawaki amesema wakati wa kumkabidhi  mkandarasi Lunyalula Construction CO. Ltd ujenzi wa daraja la Mfilisi katika kijiji cha Iyombwe  lenye urefu wa mita 21.75 na upana wa mita saba.

Mhandisi Sawaki amesema  kuwa ,muda wa mkataba wa mradi huo ni siku 240 kuanzia Oktoba 12, 2023 hadi Juni 8, 2024 chini ya usimamizi wa Tarura Wilaya ya Kilosa.

Meneja wa Tarura Wilaya ya Kilosa amesema kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Wilaya imetenga fedha kwa ajili ya matengenezo ya barabara na madaraja ambao  jumla ya miradi  nane yenye thamani ya Sh bilioni 4.

7 itatekelezwa.

“Katika miradi hiyo upo wa ujenzi wa daraja la mto  Mfilisi lenye urefu wa mita 21.

75 na upana wa mita saba “ amesema  Mhandisi Sawaki

Naye Mbunge wa Jimbo la Mikumi, Dennis Londo ameishukuru  Serikali ya awamu ya sita kwa kutoa fedha nyingi kwa Wakala huo ili uweze  kuhudumia barabara na madaraja maeneo ya vijijini  na mijini  kwa lengo la kuboresha utoaji huduma za kijamii na za kiuchumi.

Nao baadhi ya wananchi wa kata hizo kwa nyakati tofauti wamesema ujenzi wa daraja hilo ni ukombozi kwao na wataondokana na adha walizokuwa wanazipata ikiwemo kushindwa kusafirisha mazao kipindi cha masika.

Habari Zifananazo

Back to top button