Kilio Moro, Mtibwa wameshuka daraja

KIGOMA: Mashabiki wa Kandanda mkoani Morogoro wamepata pigo baada ya Timu ya @mtibwaofficial kushuka daraja.
Mtibwa ni moja timu zinazosifika kutengeneza wachezaji kwenye soka la Tanzania na licha ya kudumu kwenye Ligi Kuu kwa muda mrefu hatimaye wababe hao wameshuka daraja baada ya kipigo cha mabao 3-2 kutoka kwa Mashujaa Fc ya Kigoma.
Matokeo hayo yameifanya Mtibwa kusalia na alama zao 21 na hata wakishinda mchezo wa mwisho watafikisha alama 24 ambazo hazitowasaidia chochote.