Kilometa 42.1 barabara za lami kujengwa Kigamboni
DAR ES SALAAM: MRADI wa Uendelezaji Dar es Salaam Awamu ya II (DMDP II) utahusisha ujenzi wa kilometa 42.1 za barabara za lami, mifereji ya maji ya mvua na madaraja katika Wilaya ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam katika mwaka 2024/2025.
Kwa mradi wote jumla unahusisha kilometa 250 za barabara zitakazojengwa Dar es Salaam. Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Zainab Katimba alibainisha hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Dk Faustine Ndugulile (CCM) lililoulizwa kwa niaba yake na Mbunge wa Viti Maalumu, Maryam Kisangi (CCM) la kutaka kufahamu mkakati wa serikali kuongeza wigo wa barabara za lami katika Wilaya ya Kigamboni.
Katimba alisema, “mradi huu kupitia mkopo kutoka Benki ya Dunia unagharimu Dola za Marekani milioni 438 na utaleta tija kubwa sana Kigamboni. Hadi sasa mradi huo upo katika hatua za usanifu.
“Serikali inatambua umuhimu wa ujenzi wa barabara za lami katika miji, hivyo itaendelea kujenga barabara hizo zikiwemo za Manispaa ya Kigamboni kulingana na upatikanaji wa fedha,” alisema. Katimba
Alisema mwaka 2024/2025 zimetengwa Sh bilioni 2.215 ambazo zitatumika kujenga barabara ya Rombo Bar – RC Church Kivukoni, Kivukoni P/S na umaliziaji wa barabara ya Chagani – Polisi kwa kiwango cha lami kilometa 1.52 na mifereji yenye urefu wa meta 3,040. Alisema kwa mwaka 2023/2024.
Serikali kupitia Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) ilitenga Sh bilioni 2.88 ambazo zilitumika kujenga barabara ya Tungi – Mjimwema na Chagani Polisi (kilometa 2.3) na mifereji yenye urefu wa meta 3,800.
Katika swali la nyongeza, Kisangi alitaka kufahamu mpango wa serikali kuhakikisha barabara za Kigamboni zinapitika ikiwemo ya Mji Mwema hadi Pemba Mnazi ambayo haipitiki kabisa na kusababisha daladala kupandisha nauli.
Pia aliuliza, “mzunguko wa lami Kigamboni ni mdogo sana ukizingatia ni eneo la viwanda na linakuwa kiuchumi, je, serikali ina mkakati gani kujenga ili wawekezaji wetu wafanye kazi vizuri?
”
Akijibu Katimba alimuagiza Meneja wa Tarura Wilaya ya Kigamboni afanye tathmini maeneo hayo maana kipaumbele cha serikali ni kurudisha mawasiliano maeneo yasiyo na mawasiliano. Alitaka meneja huyo aende maeneo ya Mji Mwema, Kibada na Pemba