Kim Jong Un akutana na Putin nchini Urusi na kuacha maswali
URUSI, Moscow,Rais wa Urusi, Vladimir Putin amekutana na Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un katika mkutano uliojadili masuala ya kijeshi, vita vya Ukraine na uwezekano wa msaada wa Urusi kwa ajili ya mpango wa siri wa satelaiti wa nchi za Kikomunisti.
–
Putin alimwonesha Kim karibu na eneo la juu zaidi la kurushia roketi za anga za juu nchini Urusi katika Mashariki ya mbali ya Urusi baada ya Kim kuwasili kwa treni kutoka Korea Kaskazini. Kim aliuliza maswali mengi ya kina kuhusu roketi huku Putin akimuonesha maeneo ya usanikishaji wa vyombo yaliyopo Vostochny na Cosmodrome.
–
Baada ya ziara hiyo, Putin mwenye umri wa miaka 70, na Kim mwenye miaka 39, walifanya mazungumzo kwa saa kadhaa na mawaziri wao na kisha kufuatiwa na mlo wa mchana wa maandazi ya Kirusi “pelmeni” yaliyotengenezwa na kaa wa Kamchatka, kisha samaki aina ya sturgeon pia uyoga. na viazi.
–
Kim aliinua bilauri ya divai ya kumtakia afya njema Putin, huku kwa pamoja wakisherehekea urafiki wao, sambamba na hayo, akatabiri ushindi kwa Urusi katika “mapambano matakatifu” na Magharibi katika vita vya Ukraine.
–
“Ninaamini kabisa jeshi la kishujaa la Urusi na watu wake watarithi ushindi na mila zao kwa uzuri na kuonesha kwa nguvu utu na heshima yao katika nyanja mbili, ile ya operesheni za kijeshi na kujenga taifa lenye nguvu,” Kim alimwambia Putin.
“Jeshi la Urusi na watu hakika watapata ushindi mkubwa katika pambano takatifu la kuadhibu uovu mkubwa unaodai uzushi na kulisha udanganyifu wa upanuzi,” Kim alisema angali ameinua bilauri yake.
–
Maafisa wa Marekani na Korea Kusini wameelezea wasiwasi wao kwamba, Kim atatoa silaha na risasi kwa Urusi, ambayo imetumia hifadhi kubwa kwa zaidi ya miezi 18 ya vita nchini Ukraine. Moscow na Pyongyang zimekanusha nia hiyo.
–
Putin alitoa vidokezo vingi kwamba ushirikiano wa kijeshi ulijadiliwa lakini alifichua maelezo machache. Hata hivyo Waziri wa Ulinzi wa Urusi, Sergei Shoigu alihudhuria mazungumzo hayo ambapo, serikali ya Kremlin ilisema majirani wanajadili masuala nyeti ambayo si ya kujadiliwa hadharani.
–
Alipoulizwa na vyombo vya habari vya Urusi, ambao walipewa nafasi kubwa katika mkutano huo, ikiwa Urusi ingemsaidia Kim kutengeneza satelaiti, Putin amesema “Hii ndio sababu ya sisi kuwepo hapa.”