URUSI: KIONGOZI wa Korea Kusini, Kim Jong amepanga kwenda Urusi kuonana na Rais Vladimir Putin kujadili uwezekano wa kuwaongeza silaha kukabiliana na Ukraine, gazeti la New York Times wameripoti.
–
“Kama tulivyoonya hadharani, mazungumzo ya silaha kati ya Urusi na DPRK yanaendelea kikamilifu,” Watson alisema, akitumia kifupi cha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea, au Korea Kaskazini.” Alisema msemaji wa usalama wa taifa wa White House, John Kirby.
–
Wiki iliyopita Ikulu ya White House ilisema Urusi ilikuwa katika mazungumzo ya siri, yenye nguvu na Korea Kaskazini ili kupata aina mbalimbali za silaha na vifaa kwa ajili ya vita vya Moscow nchini Ukraine.
–
Kim atasafiri kutoka Pyongyang kwa treni ya kivita, hadi Vladivostok kwenye Pwani ya Pasifiki ya Urusi, ambako atakutana na Putin, gazeti hilo lilisema.
–
Safari hiyo imekuja wakati Urusi ikijadili kufanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi na Korea Kaskazini baada ya Waziri wa Ulinzi wa Urusi, Sergei Shoigu kujaribu katika ziara ya Korea Kaskazini kuishawishi Pyongyang kuiuzia Urusi kutumia risasi za kivita.