Kim Poulsen atupiwa virago Stars

Kim Poulsen atupiwa virago Stars

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Taifa ‘Taifa Stars’, Kim Poulsen ameondolewa katika nafasi hiyo.

Taarifa iliyolewa leo na Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Clifford Ndimbo, imesema uamuzi wa kumuondoa Kim umefikiwa baada ya makubaliano ya pamoja ya pande hizo mbili. Poulsen sasa atabaki na timu za Taifa za vijana.

Kutokana na mazingira hayo, Taifa Stars itakuwa chini ya kocha wa muda, Hanour Janza, akisaidiwa na Mecky Maxime na Juma Kaseja.

Advertisement

Taifa Stars jana ilifungwa na Uganda ‘The Cranes’ bao 0-1 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, mchezo wa kuwania kufuzu fainali za CHAN. Timu hizo zitarudiana mwishoni mwa wiki hii nchini Uganda.