Kinana apewa uchifu

MACHIFU wa Tabora wamemsimika uchifu wa unyanyembe Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Abdulrahman Kinana ili amsaidie Chifu Mkuu Hangaya Rais Samia Suluhu Hassan katika majukumu yake ikiwemo ya uchifu.

Kinana amepewa jina la Chifu Kiyungi jina la baba ake Chifu Isike mwana wa Kiyungi.

Akimsimka uchifu huo, Chifu Nsagata Fundikira Ngulai ambae ni Chifu wa Tabora nzima, amesema wamempa uchifu huo kutokana na kuwa kiungo muhimu ndani ya Chama Cha Mapinduzi.

Aidha, alimkabidhi vazi jekundu anbalo linamaanisha Mamlaka na kumvisha pia vazi jeupe ambalo ameelezea kuwa linamaanisha amani na upatanishi.

“Wewe ni kiongozi mzuri, umekua mpatanishi siku zote, wewe ni kiungo muhimu ndani ya Chama na nje ya Chama Cha Mapinduzi, Chifu Hangaya ni Chifu Mkuu wa Machifu wote Tanzania nzima, na wewe utakua msaidie Mkuu wa Chifu Hangaya.” Amesema na kuongeza.

” Kuanzia leo wewe ni Chifu wa Unyanyembe, hakuna atakaekugusa, yeyote atakagombana na wewe au kukujaribu ajue atapambana na wanyanyembe wote.” Amesem

Zoezi hilo la kumsimika kuwa Chifu Msaidie Mkuu limefanyika katika uwanja wa Chipukizi mkoani Tabora.

Habari Zifananazo

Back to top button