Kinana ataja mambo 4 ziara mikoani

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana, ametaja mambo manne yaliyomleta mikoa ya Kigoma, Kagera, Mwanza na Geita.

Kinana amesema ziara yake katika mikoa hiyo inalenga kusikiliza kero za wananchi, kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM, kuangalia mwenendo wa uchaguzi ndani ya chama na kuwatia moyo wana CCM.

Ametoa kauli hiyo leo Septemba Mosi, 2022 akiwa Uwanja wa Ndege wa Kigoma alipowasilia akitokea jijini Dar es Salaam, katika ziara ambayo ameambatana na Katibu wa Siasa, Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya CCM, Shaka Hamdu Shaka.

Viongozi hao wamepokelewa na Mkuu wa Mkoa Kigoma,Thobias Andengenye na viongozi wa CCM wakiwemo wabunge.

“Ni ziara ya kawaida ambayo inalenga kusikiliza kero, kukagua utekelezaji wa ilani, kuangalia mwenendo wa uchaguzi wa chama na kuwatia moyo wana CCM wenzetu,” amesema Kinana.

Mkoani Kigoma viongozi wa CCM watakagua Bandari Ujiji na kuangalia ukarabati wa Meli ya Mv Sangara kisha kuzungumza na wana CCM.

Habari Zifananazo

Back to top button