Kinana ateta na Rais wa Vietnam.
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Abdulrahman Kinana ameongoza ujumbe wa CCM kwenye mazungumzo na Rais wa Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Vo Van Thuong, jijini Ha Noi, Viet Nam.
Katika mazungumzo hayo, Kinana aliwasilisha ujumbe maalum kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, wa kuhimiza ushirikiano wa kiuchumi baina ya nchiĀ hizo mbili ili kuwanufaisha wananchi wa Tanzania na Vietnam.