Kinana: Gen. Musuguri ni mzalendo wa kweli
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amemtembelea Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali David Musuguri nyumbani kwake Butiama mkoani Mara na kumjulia hali.
Akiwa nyumbani kwake, Kinana amemuelezea Jenerali Musuguri kuwa ni mzalendo wa kweli aliyeongoza vita ya Kagera uliyochukua kipindi kifupi kuliko vita vyote duniani.
Amesema, vita hiyo ilianza Novemba 11, mwaka 1978 hadi Aprili 1979.
“Jenerali Musuguri ameliongoza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa zaidi ya miaka 50, ameliongoza Jeshi katika nafasi mbalimbali, tukiadhimisha miaka 44 ya vita ya Uganda Jenerali Musuguri ndiye aliyeyaongoza majeshi ya Tanzania kumng’oa Nduli Idd Amin.
Awali, Jenerali Musuguri alionyesha kufurahia ujio wa Makamu huyo wa CCM na pia alimuwekea mikono kichwani kama hishara ya kumbariki.
Januari 5, 2023 Jenerali Musuguri ametimiza umri wa miaka 103.