Kinana: Jukumu la kujiendeleza ni binafsi

Serikali inatengeza tu fursa

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana, amesema kuwa jukumu la kujiendeleza ni la mtu binafsi na hakuna anaeweza kumwendeleza mtu mwingine.
Amesema,  hata serikali haiendelezi watu bali hutengeneza  mazingira mazuri kwa wananchi kujiendeleza kupitia  fursa mbalimbali.
Kinana ameyasema hayo  wakati akizingumza na waganga wa tiba asiili Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu ambapo amewapongeza kwa kazi nzuri wanazofanya katika kushiriki kwenye shughuli za maendeleo.
Amesema, serikali inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imeendelea kutengeneza mazingira mazuri na kupanua fursa za wananchi kufanya shughuli mbalimbali huku akisisitiza kuwa sasa kuna uhuru mkubwa wa watu kujieleza na kutoa maoni yao.
“Watu wanajiendeleza wenyewe, kazi ya serikali ni kutengeneza mazingira mazuri kwa wananchi kutafuta fursa wajiendeleze kama ni kilimo, kama ni biashara, kama ni ujasiriamali, kama nia ajira, kila mtu kwa nafasi yake anajiendeleza mwenyewe , hakuna mtu anayemuendeleza mwingine,” amesema na kuongeza
“Jambo hili limekuwepo tangu Awamu ya kwanza chini ya uongozi wa Baba wa Taifa, Julius Nyerere na ndio hivyo hivyo hadi leo chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan. Ninyi ni mashahidi tangu Rais ameingia madarakani kazi moja kubwa aliyoifanya ni kupanua uhuru.
Nyinyi ni mashahidi, Tanzania ya leo watu wana uhuru mkubwa , haki imepanuliwa, haki ya kuishi imepanuliwa zaidi, haki  ya kutoa maoni imepanuliwa zaidi, haki ya kusikilizwa imeheshimiwa zaidi, ndio maana watanzania leo wana nafasi kubwa ya kutoa maoni yao. ” Amesema Kinana na kusisitiza.
” Nirudie tena maendeleo ya mtu yanaletwa na mtu mwenyewe, serikali haileti maendeleo, mara nyingi serikali inashughulika kujenga maendeleo ya vitu ambavyo inamrahisishia mwananchi kufanya shughuli zake kwa urahisi zaidi kama kujenga miundombinu ya barabara Vituo vya Afya, shule ili wananchi wapate fursa ya kujiendeleza.
Aidha, Kinana amesema amefurahishwa na Waganga wa Tiba Asili kwa kuwa wanafanya uganga wao kisasa na kwenda na wakati
“Tunaambiwa hapa, watoto wenu wanakwenda shule, watoto wenu wanasoma, wanafanya kazi katika serikali na katika jamii, lakini vile vile mmejitoa katika kuleta maendeleo ya jamii, kujenga shule, kujenga vituo vya afya, kujenga kituo cha Polisi, ndio tofauti ya Waganga wa Tiba Asili na wachawi.
“Mngekua mnaitwa wachawi kusingekua na haja ya kujenga kituo cha Polisi, mngemalizana wenyewe kichawi.”Amesema
Amewapongeza kwa kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii na wote  ni wakulima wa mazao mbali mbali ikiwemo Ufuta, Pamba , na mazao mengine na kwamba hawakai  kusubiri kutibu.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Elsa J. Clark
Elsa J. Clark
1 month ago

Single Mom With 4 Kids Lost Her Job But Was Able To Stay On Top By Banking Continuously DOLLER 1500 Per Week With An Online Work She Found Over The Internet
.
.
.
Check The Details HERE_____ https://Fastinccome.blogspot.Com/

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x