Kinana: Maisha ni hadithi

Simulizi nzuri zinaishi

ARUSHA: Makamu Mwenyekiti wa CCM, Tanzania Bara,Abdulrahman Kinana amesema maisha ni hadithi hivyo ukitaka kuandika maisha yako uwe na mambo mema kwani uongozi ni tabia si akili na wala si masomo.

“Kinachomtofautisha mtu katika uongozi ni tabia yake kwani kiongozi ni mtu anayejenga umoja”
 
Kauli hiyo imetoa katika Ibada ya Kumuaga aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Arusha, marehemu Zelothe Stephen ambapo amesema
 
Cheo cha marehemu kilikuwa cha juu sana lakini hakuwa kiongozi wa kutisha watu na watu walimheshimu kwa tabia na alitoa rai kwa viongozi wengine kuweka mkazo katika tabia na si vyeo vyao.
 
“Mungu atufanye kuwa watu wenye tabia njema na si ukubwa wa vyeo” amesema Kinana.
 
Huku Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella akisema amepoteza mtu muhimu katika maisha yake na alikuwa ni kiongozi wa pekee.

Habari Zifananazo

3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button