MTANDAO: SIMBA SC imekamilisha usajili wa kiungo, Saleh Karabaka (23) kutoka JKU ya Zanzibar kwa mkataba wa miaka mitatu.
Taarifa ya usajili wa Karabaka imetangazwa kupitia tovuti ya klabu hiyo, mchana wa Januari Mosi, 2024 na unakuwa usajili wakwanza wa klabu hiyo katika dirisha hili dogo.
“Karabaka tayari amejiunga na timu visiwani Zanzibar na ataanza kuonekana akiwa na jezi ya Mnyama katika michuano ya Mapinduzi inayoendelea,” imeeleza taarifa ya Simba SC.
Taarifa ya Simba SC inaeleza kuwa mbali na uwezo alionao Karabaka jambo jingine lililoivutia klabu hiyo ni umri mdogo ambao wanaamini atakuwa msaada mkubwa kwa timu.
“Mchezaji chipuki ni hazina yetu kubwa na hakuna sehemu bora ya kumtambulisha zaidi ya aliyozaliwa na kukuza kipaji chake ambayo ni Zanzibar.
” Imeeleza taarifa hiyo.