RAIS Samia Suluhu Hassan amemteua Waziri Kindamba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART).
Kindamba anachukua nafasi ya Gilliard Wilson Ngewe ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Kabla ya uteuzi huo, Kindamba alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga.