DAR ES SALAAM: Msanii wa Bongo fleva nchini Ali Kiba ‘King Kiba’ ameongoza wasanii wenzake kuchangia taasisi ya Profesa Jay Foundation ya msanii wa Hip Hop nchini, Joseph Haule.
Ali Kiba amechangia kiasi cha Sh milioni 5 ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Prof Jay katika ustawi wa taasisi hiyo itakayoshughulika na wagonjwa wa figo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa taasisi hiyo Kiba amesema kuwa Kings music watachangia milioni 5 na mashabiki wa King waliweza kuchangia laki tano.
Wasanii wengine ni pamoja na Judith Wambura Lady Jay Dee amechangia kiasi cha Sh millioni 2, Gabo, JB, Batuli nao wamechangia Sh milion 3, Weusi wamechangia Sh milioni 1 pamoja na Chege na Temba milioni 1 na laki 7.