Kinondoni kukosa umeme

WAKAZI wa Mkoa wa Kinondoni Kaskazini, hususan maeneo ya Mikocheni na vitongoji vyake, watakosa huduma ya umeme kwa muda mfupi kutokana na matengenezo yanayopangwa kufanyika katika kituo cha kupoza umeme cha Oysterbay.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Shirika la Umeme Tanzania, huduma ya umeme itasitishwa Jumatano, Februari 28, 2024, kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni.

Aidha miongoni mwa maeneo yatakayoathirika kwa kukosekana kwa huduma ya umeme ni pamoja na Oysterbay, Kinondoni, Drive inn, Namanga, Makangira, Uwanja wa Magunia, Albin said, Uganda avenue, Msasani tower, Galilaya, Msasani Peninsula, Mayfair plaza, Shoppers, Bonde la Mpunga, TMJ Hospital, Highland villas na baadhi ya maeneo ya jirani.

Lengo la matengenezo haya ni kuboresha miundombinu ya umeme na hivyo kuimarisha upatikanaji wa huduma kwa wateja.

Habari Zifananazo

Back to top button