Kiongozi mbio za Mwenge ahimiza kuendelea kuhesabiwa

KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Sahil Geraruma, amewahimiza Watanzania kuendelea kujitokeza kuhesabiwa kwenye Sensa ya Watu na Makazi.

Sensa hiyo imeanza kufanyika tangu Agosti 23, mwaka huu.

Gareruma alitoa rai hiyo katika nyakati tofauti wilayani Gairo, mkoani Morogoro kwenye ujumbe Mwenge wa Uhuru ambao mbio zake mkoani humo zilianza Agosti 24, mwaka huu baada ya kukabidhiwa toka Mkoa wa Dodoma.

Advertisement

Kaulimbiu ya Mbio za Mwenge kwa mwaka 2022 ni “Sensa ni Msingi wa Mipango ya Maendeleo: Shiriki kuhesabiwa, tuyafikie Maendeleo ya Taifa”.

Licha ya kaulimbiu hiyo, mbio hizo zinaendelea kuelimisha na kuihamasisha jamii ya Watanzania kuhusu umuhimu na uzingatiaji wa lishe bora, mapambano dhidi ya rushwa, mapambano dhidi ya VVU/Ukimwi, mapambano dhidi ya matumizi ya mihadarati pamoja na malaria.

Kwa upande mwingine Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Albert Msando aliwataka wananchi wa wilaya hiyo wajikite kwenye sensa kwa siku zote zinazotumika kuhesabu.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Malinyi, Antipas Mgungusi alisema alishahesabiwa siku ya kwanza hivyo aliwataka wananchi wake kuendelea kujitokeza na kutoa ushirikiano kwa makarani wa sensa.

 

/* */