Kiongozi Mkuu wa Iran aongoza ibada mazishi ya Rais wa Iran

Tehran, IRAN: KIONGOZI Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei ameongoza sala katika hafla ya kumbukumbu ya marehemu Rais wa Iran Ebrahim Raisi na wapambe wake waliofariki katika ajali ya helikopta iliyotokea Jumapili nchini humo.

“Ee Mwenyezi Mungu, hatukuona lolote ila jema kutoka kwake,” alisema Khamenei siku, akitoa heshima kwa Raisi katika Chuo Kikuu cha Tehran mbele ya maelfu ya watu, ambao walitembea kwa miguu kutoka Enghelab (Mapinduzi) Square hadi Azadi (Uhuru).

Majeneza ya Raisi, aliyekuwa na umri wa miaka 63, na wengine saba waliofariki katika ajali hiyo Jumapili, likiwemo la Waziri wa Mambo ya Nje wan chi hiyo Hossein Amirabdollahian, yalipambwa kwa bendera za Iran na picha zao.

“Barabara zimefungwa kabisa kwa trafiki, pamoja na tahadhali za kiusalama zilichukuliwa, vituo kadhaa vya ukaguzi na watu wengi wamejitokeza kumzika Rais huyo na wenzake waliofariki katika ajali ya helkopta.” Resul Serdar wa Al Jazeera, akiripoti kutoka Freedom Square, alisema kuna ulinzi mkali katika eneo hilo.

Wageni waliofika katika hafla ya kumuaga Rais huyo ni pamoja na kiongozi wa kisiasa wa Hamas Ismail Haniyeh, Makamu wa rais wa Uturuki na Waziri wa Mambo ya Nje, Naibu Waziri Mkuu wa India, Mkuu wa Duma ya Urusi, Waziri Mkuu wa Iraq na wawakilishi wa Taliban kutoka Afghanistan.

“Ninakuja kwa jina la watu wa Palestina, kwa jina la makundi ya upinzani ya Gaza … kutoa rambirambi zetu,” Haniyeh aliwaambia wale waliokusanyika. Amesimulia kuwa alikutana na Raisi mjini Tehran wakati wa Ramadhani na alimsikia marehemu rais akisema Palestina ndio suala kuu la ulimwengu wa Kiislamu.

Khamenei ametangaza siku tano za maombolezo ya kitaifa nchini humo. Kumbukumbu za Raisi na wasaidizi wake zilianza siku ya Jumanne katika mji wa Tabriz na kituo cha makasisi wa Shia cha Qom.

Kufuatia msafara wa Jumatano, mwili wa Raisi utapelekwa katika mji aliozaliwa wa Mashhad kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, ambapo atazikwa baada ya ibada ya mazishi katika Madhabahu ya Imam Reza.

Mabaki ya wengine waliofariki katika ajali hiyo pia yatatumwa katika miji yao ili kuzikwa.

Habari Zifananazo

Back to top button