Kiongozi Simba amchangia Feisal aende CAS

Kiongozi Simba amchangia Feisal aende CAS

ADUI muombee jana: Baada ya jana kiungo Feisal Salum ‘Feitoto’ katangaza mashabiki wake na mashabiki wa mpira wa miguu nchini wamchangie ili afungue kesi dhidi ya Yanga katika Mahakama ya Michezo ya Kimataifa (CAS), fasta tu leo Meneja Habari na Mawasiliano Klabu ya Simba, Ahmed Ally amemtumbukizia Sh 20,000.

Kupitia mitandao ya kijamii leo Mei 26, 2023, Ahmed ameanzisha kampeni aliyoibatiza jina Okoa Kipaji, yenye lengo la kuunga mkono ombi la Feitoto kwa wapenzi wa mpira wa miguu kumchangia mchezaji huyo, ili kufanikisha azma yake.

“Okoa kipaji cha fundi @194. Semaji nimetimiza wajibu wangu,” ameandika Ahmed Ally.

Advertisement

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *