Kiongozi upinzani jela miaka mitatu

MAHAKAMA nchini Tunisia imemhukumu kiongozi wa upinzani Rached Ghannouchi, mkosoaji mkali wa Rais Kais Saied, kifungo cha miaka mitatu jela kwa tuhuma za kukubali ufadhili kutoka nje, wakili wake amesema.

Ghannouchi, 82, mkuu wa chama kikuu cha upinzani cha Ennahda, amekuwa gerezani tangu Aprili. Mwaka jana alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa tuhuma za uchochezi dhidi ya polisi.

Wakili wake aliongeza kuwa mahakama pia ilimfunga mkwe wa Ghannouchi Rafik Abdessalem ambaye ni ofisa mkuu wa Ennahda, kifungo cha miaka mitatu jela katika kesi hiyo hiyo, pamoja na kukitoza faini chama cha Kiislamu cha Dola milioni 1.1.

Mwaka jana, mamlaka ya Tunisia ilipiga marufuku mikutano katika ofisi zote za Ennahda na polisi walifunga makao makuu ya Salvation Front, muungano mkuu wa upinzani, katika kile ambacho baadhi ya makundi yalikiita marufuku ya ukweli.

Habari Zifananazo

Back to top button