KIONGOZI mkuu wa wanamgambo wa Al-Shabaab, Maalim Ayman ameuawa na vikosi vya Somalia na Marekani.
Taarifa hizo zinakuja ikielezwa kuwa kiongozi huyo na kundi lake walipanga kufanya mashambulizi nchini Somalia na Kenya, Waziri wa Habari wa Somalia alisema.
“Imethibitishwa Maalim Ayman ameuawa katika operesheni ya pamoja ya Jeshi la Somalia kwa usaidizi wa vikosi vya Marekani tarehe 17 Disemba,” Daud Aweis alisema. “Ayman aliwajibika kwa kupanga mashambulizi mabaya ya kigaidi nchini Somalia na nchi jirani.”
Kamandi ya jeshi la Marekani Afrika (AFRICOM) ilifanya shambulizi la anga, msemaji wa AFRICOM alisema. Mgomo huo ulifanywa dhidi ya kundi la wanamgambo karibu na mji wa Jilib kusini mwa Somalia.
Ayman alikuwa kwenye orodha ya wanaotafutwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani huku zawadi ya Dola milioni 10 ikitolewa kwa taarifa zitakazopelekea kukamatwa kwake.
Comments are closed.