Kiongozi wa kijeshi Gabon aapishwa kuwa rais

GABON: Kiongozi wa kijeshi nchini Gabon, Brice Nguema, ameapishwa kuwa rais wa mpito wa taifa hilo.

Jenerali Nguema aliongoza mapinduzi ya Jumatano iliyopita dhidi ya aliyekuwa Rais wa chi hiyo Ali Bongo, muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi uliogubikwa na utata.

Katika hafla hiyo, umati wa raia waliojitokeza kushuhudia kuapishwa kwake walihanikiza kwa nderemo na vifijo kama ishara ya uungaji mkono kwa uongozi mpya.

Hata hivyo, kuna wasiwasi kwamba utawala wa Jenerali Nguema utakuwa mwendelezo wa nasaba ya Rais Bongo iliyodumu kwa miaka 55 kwani inaelezwa Bongo na Nguema ni mabinamu.

Ali ni motto wa kiongozi wa zamani wa taifa hilo, Omar Bongo aliyekalia kiti cha urais kwa miaka 41 kabla ya kufariki mwaka 2009 na kurithiwa na mwanawe Ali Bongo ambaye naye aliongoza taifa hilo kwa miaka 14.

Habari Zifananazo

Back to top button