Kishimba ataka Wizara ya matumizi na kero

Ahoji serikali kurudi kwenye biashara

MBUNGE wa Kahama Mjini (CCM), Jumanne Kishimba ametoa ombi la serikali kuongeza Wizara ya Matumizi na Kero na CAG na Takukuru wahusishwe kabla ya fedha kupelekwa kwenye miradi.

Kishimba ameyasema hayo leo wakati akichangia hotuba ya ofisi ya Waziri Mkuu, ambapo amesema kuna umuhimu wa serikali kuunda wizara hiyo ili ishughulikie na uchambuzi wa miradi kabla ya  fedha kutolewa.

“Wizara hii ya matumizi na kero iundwe kuangalia mradi unafaaa au haufai, CAG,Takukuru wauangalie  kabla ya pesa kupelekwa.”Amesema na kuongeza

Mbwa anabweka wakati wa mwizi ili asiibie sasa kashaiba anabweka…inasaidia nini, hapa sisi tunajadili ufisadi uliofanywa katika taasisi za serikali, tunabweka tu, haitasaidia, CAG, Takukuru  wawe wanahusishwa katika kila miradi ili kuzuia ufisadi, wabweke kabla wizi haujatokea.”Amesema Kishimba

Aidha, ametolea mfano stendi za mabasi na masoko ambayo yamejengwa kwa fedha nyingi za walipa kodi na matokeo yake hazifanyi vizuri kutokana na kukosa wateja

“Stedi mmejenga nje yam ji, mnalazimisha abiria lazima akashuke stendi, badala ya nane nane, alafu achukue tena usafiri kwa sh 5,000 umejenga mradi kwa pesa za wananchi alafu bado tena mnawadhibu kwa kuwalazimisha hii sio sawa.” Amesema na kuongeza

‘Mmejenga masoko ya ghorafa kwa sh Bilioni 40 matokeo yake masoko yamekosa wateja, hivi nani atapanda ghorofani kwenda kununua nyanya, miradi kama hii ilipaswa kuchambuliwa kwanza kama inafaa au haifai kabla ya kuingiza mabilioni ya fehda bila faida.

Aidha, ameitaka serikali kujitafakari kuhusu kurudi kufanya biashara ambayo ilishindwa miaka ya 60 na 80.

Serikali inataka kurudi kwenye biashara kile kilichowafanya wakaachana na kufanya biashara kimesharekebishwa? Kama wale wa miaka ya 60 na 80 walishindwa na walikuwa wanakula mihogo je hawa wa blue band wataweza?

“Leo ukiona matajiri hakuna mzima wote wa na matatizo ya gauti wengine presha, serikalini mnastaafu miaka 60 je mnataka kumuangushia nani huo mzigo?

Mnataka kuingia kwenye biashara kabla biashara haijaanza nusu ya hela imeshailiwa, mnafanya biashara gani? alihoji

 

Habari Zifananazo

Back to top button