Kitambaa Cheupe, Liquid, Wavuvi Camp zafungwa

Mkurugenzi wa NEMC Samuel Gwamaka

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEC), limefungia baa zaidi ya 80 ikiwemo Wavuvi Camp iliyopo Coco Beach, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Nyingine zilizofungiwa ni Element Masaki, Boardroom,  Kitambaa Cheupe, Liquid, Warehouse na Soweto kwa upande wa Dar es Salaam

Dodoma wameifungia baa ya  Chako ni Chako na Rainbow wakati Mwanza wameifungia Gentleman na  The cask.

Advertisement

Mkurugenzi wa NEMC Samuel Gwamaka akizungumza leo Mei 8, 2023 jijini Dar es Salaam amesema wamechukua hatua ya kufungia baa hizo maarufu baada ya kukuta kelele zilizopo kinyume cha sheria ya usimamizi wa mazingira namba 20 ya mwaka 2004 na kanuni ya viwango vya udhibiti wa kelele na mitetemo ya mwaka 2015.

Amesema, biashara ambayo inazunguka maeneo ya watu kelele zinatakiwa kuwa 60DBA nyakati za mchana na 40 nyakati za usiku.

“Wengi tuliwapa faini lakini waliendelea kukaidi, tumefungia baa19 za wilaya ya Kinondoni, Ilala 25, Kigamboni 22, Temeke baa 12, Dodoma 5 na Mwanza 6,” Amesema Gwamaka.

Amesema, baadhi ya baa licha ya kupewa onyo mara kadhaa lakini ziliendelea kukaidi.

“Kuna Baa zinatusumbua saba na wamekua sugu, hao ni Wavuvi Camp, Boardroom, Warehouse, Kitambaa Cheupe, Element, Soweto, Liquid, Chako ni Chako, Rainbow, Gentleman na Cask ya Mwanza,” amesema Gwamaka na kuongeza:

“Hawa  tumechukua hatua ya kuzifungia kwa kuwa tumewaonya mara nyingi sana, lakini hawasikii. Tumewafungia tayari wameshakuja kuomba wasamehewe na wafunguliwe, ” amesema.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *