Kitenge kina raha yake mwilini

DAR ES SALAAM;  ULIMWENGU wa mitindo ya mavazi ya Afrika, huwezi kukosa mavazi yaliyoshonwa kwa kutumia kitenge. Kitenge kimekuwa ni vazi maalumu linalomtambulisha mwafrika yoyote anapokuwa amevaa mahali popote duniani.

Kitenge kinaweza kushonwa katika mitindo tofauti na kuvaliwa na watu wote, watoto, vijana, wakubwa, wanawake na wanaume na kuonekana nadhifu machoni pa watu.

Advertisement

Kupendeza ni jambo kubwa, ambalo wanamitindo na watu wanaopenda kwenda na wakati hulizingatia. Vazi la kitenge pamoja na kumfanya mvaaji kupendeza na kuvutia, lakini pia humletea heshima mvaaji popote anapoingia.

Vazi hilo linaweza kuvaliwa katika mikutano yoyote mikubwa, sehemu za ibada, kazini na hata katika sherehe mbalimbali.

Baadhi ya watu maaarufu wanaonekana wanavyotokelezea na vazi la kitenge, huku wakijipatia heshima kubwa. Mataifa yanayosifika kwa kuwa na vitenge vizuri licha ya Tanzania  ni Congo DRC, Nigeria na Ghana.