MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Mary Chatanda amesema Kituo cha Afya cha Maili tano katika wilaya Tabora Mjini kitajengewa kisima kuondokana na changamoto ya maji iliyopo kwa sasa.
Chatanda amesema hayo leo baada ya kutembelea kituo hicho na kufurahishwa na ujenzi wa wodi ya mama na mtoto katika kituo hicho.
” Nimefurahishwa na ujenzi huu lakini kuna changamoto ya maji katika kituo hiki, nimempigia Naibu Waziri Marryprisca Mahundi na kuniahidi atachimba kisima hapa hivi karibuni na itakuwa mwisho wa changamoto ya maji katika Kituo hiki, “amesema.
Ameeleza kuwa ameona aanze na la maji kwa kuwa wanawake wengi wanaojifungua katika kituo hicho lazima watakuwa wanapata shida sana katika kupata maji safi na salama, hivyo sasa wanawake na wananchi Maili Tano changamoto ya maji itaisha.