Kituo cha biashara EAC kuanza kazi Juni

DAR ES SALAAM; ZAIDI ya wafanyabiashara 2000 wanatarajia kunufaika na Kituo cha Biashara cha Afrika Mashariki kilichopo Ubungo jijini Dar es Salaam kitakachoanza kutumika Juni mwakani.

Kituo hicho ambacho kitafanya kazi saa 24, kimefikia asilimia 70 ya utekelezaji wa ujenzi wake, ambapo kinatarajia kugharimu dola za Marekani milioni 118 kitakapokamilika.

Akizungumza katika ziara ya kutembelea kituo hicho, Mkurugenzi Mtendaji kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Elias Ntiruhungwa amesema mradi huo utakuwa na maduka 2000, utanufaisha wafanyabiashara wa Tanzania, Afrika Mashariki na nchi nyingine.

Amesema hadi kufikia Desemba mwaka huu, kazi zote zitakuwa zimekamilika na ifikapo Juni mwakani kituo hicho kitaanza kutumika rasmi.

“Kutakuwa na biashara mbalimbali. kuna maeneo ya benki, taasisi za kifedha, pamoja na maduka mbalimbali,” amesema.

Amesema eneo ambalo linajengwa mradi huo ni maarufu kwa kuwa kulikuwepo na mabasi yaendayo mkoani, ambapo kwa sasa stendi imehamishiwa Mbezi Mwisho.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya East Africa Commercial and Logistics Center (EACLC), Wang Xiangyu amesema mradi huu ulianza mwishoni mwa mwaka jana, wanatarajia utakamilika Desemba mwaka huu.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
EliseMcGhee
EliseMcGhee
16 days ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ http://Www.Careers12.com

Last edited 16 days ago by EliseMcGhee
FILI PO
FILI PO
15 days ago

Thanks for the info, just started this 4 weeks ago. I’ve got my FIRST check total of $350, pretty cooll.!

Work At Home Special Report! (financereports.online)

Back to top button
2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x