DAR ES SALAAM: JINA la Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli kilichopo Mbezi jijini Dar es Salaam halijabadilishwa.
Kumetokea sintofahamu katika taarifa yetu iliyochapishwa Desemba 16, 2023 kuhusu mapato ndani ya kituo hicho ambapo pasipo kukusudia ilitumika picha isiyo sahihi.
Tunapenda kuutaarifu Umma kuwa hakuna mabadiliko yoyote ya jina katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli.
Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza kutokana na taarifa hiyo.
Comments are closed.