KIUNGO wa TS Galaxy ya Afrika Kusini, Bernad Parker amevunjwa mguu na kiungo wa Mamelod Sundowns, Bogani Zungu katika mchezo wa kombe la Carling Cup uliopigwa usiku wa leo.
Zungu alioneshwa kadi nyekundu dakika ya 58 baada ya kumkanyaga mchezaji huyo katika mchezo ulioisha kwa sare ya mabao 2-2 na Galaxy kuiondoa Mamelod kwa matuta 5-4.
Haraka Parker alitolewa nje na madaktari huku akionekana kuvunjika mguu. Kiungo huyo ana umri wa miaka 37, matibabu yake huenda yakachukuwa sio chini ya miaka miwili.